phone: +420 776 223 443
e-mail: support@londoncreative.co.uk

Friday 13 March 2015

Labda hii ni mpya kwako.. mbwa anayetembea na kuvaa kama binadamu yani.. Kuna video


Mbwa kwenye pozi zake na mavazi kama tu binadamu,  pata picha unakutana naye barabarani halafu anatembea tu kama binadamu kwa miguu miwili.
Wachina hawajashindwa kitu, hii imezua mjadala katika mitandao.. waliobahatika kukutana naye barabarani walijikuta wakigeua vichwa kumcheki, imetokea China.
Mbwa huyo amevalishwa kofia, shati na sketi, mgongoni amebeba begi kama mwanafunzi wa shule, halafu anakatisha zake mtaani poa kabisa yani.


Mtu anaemfuga mbwa huyo anaitwa Zhu, amesema ametumia muda wa mwezi mmoja kumfundisha mbwa huyo kutembea kwa miguu miwili kama binadamu, ana uwezo wa kutembea kilomita mbili wima kama mwanadamu.
Zhu anasema alianza kufundisha mbwa kama njia ya kujifurahisha miaka 20 iliyopita, baada ya kuona mafanikio aliona aendelee kufanya hivyo kwa kuwafundisha mbwa wengine wengi.

No comments:

Post a Comment