phone: +420 776 223 443
e-mail: support@londoncreative.co.uk

Sunday 22 March 2015

Uliwahi kuvutiwa na uvaaji wa Pharrell Williams? Basi ile style yake imempa TUZO !!






 Nyingine ambayo huenda hujaipata ni ishu ya Pharell Williams kutajwa kuwa ndiye mwanamuziki aliyeshinda CFDA Fashion Icon Awards ambapo ushindi huo unatokana na jinsi style yake imekuwa maarufu na kushawishi watu wengi duniani......Pharell atapewa Tuzo hiyo June 1 2015, lakini toka jina lake limetajwa kama mshindi mitandao imeendelea kuandika na kuuchambua huu ushindi wa Pharell


Wapo walioandika eti kawa mshindi kwa sababu ya ile kofia ambayo anapendelea kuvaa!
Mastaa wengine waliowahi kushinda Tuzo hii ni pamoja na Rihanna na Lady Gaga.


Sunday 15 March 2015

Hanscana Ame Copy NaKu Pest Idea Ya Wimbo Wa Jux Toka Xo(Nisher)




Director Nisher aliye fanya ngoma kadhaa za video ikiwemo Xo ya Joh Makini hivi karibuni alitoa malalamiko juu ya video mpya ya Jux iliofanywa na Director Hanscana kuwa hajatumia mawazo yake na ufundi zaidi ya kuamisha mawazo toka kwenye video ya Xo ilikuwa imefanyika chini ya mikono ya nisher 
Aliamua kuthibitisha hayo kwa kupost baadhi ya picha kwenye mtandao wa picha(Instagram) na kuonesha alicho kuwa anakilalamikia 



Friday 13 March 2015

Labda hii ni mpya kwako.. mbwa anayetembea na kuvaa kama binadamu yani.. Kuna video


Mbwa kwenye pozi zake na mavazi kama tu binadamu,  pata picha unakutana naye barabarani halafu anatembea tu kama binadamu kwa miguu miwili.
Wachina hawajashindwa kitu, hii imezua mjadala katika mitandao.. waliobahatika kukutana naye barabarani walijikuta wakigeua vichwa kumcheki, imetokea China.
Mbwa huyo amevalishwa kofia, shati na sketi, mgongoni amebeba begi kama mwanafunzi wa shule, halafu anakatisha zake mtaani poa kabisa yani.


Mtu anaemfuga mbwa huyo anaitwa Zhu, amesema ametumia muda wa mwezi mmoja kumfundisha mbwa huyo kutembea kwa miguu miwili kama binadamu, ana uwezo wa kutembea kilomita mbili wima kama mwanadamu.
Zhu anasema alianza kufundisha mbwa kama njia ya kujifurahisha miaka 20 iliyopita, baada ya kuona mafanikio aliona aendelee kufanya hivyo kwa kuwafundisha mbwa wengine wengi.

Tuesday 10 March 2015

Issue Ya Hasheem Thabiti Kuto Penda Kuvaa Suluali Za Jeans





 Mchapo amazing..:Leo Pambaika inataka ikupe jibu kwa nini mkali Hasheem Thabit uwa hapendelei kuvaa jeans.. Sababu ya huyu jamaa bwana inavyosemekana uwa hapendelei kuvaa jeans kwa sababu jeans zote amezizidi urefu kwa sababu yeye ni mrefu zaidi ya foot 9 ndio maana hupendelea kuvaa suluali za vitambaa na pensi kwa sababu kitambaa inakuwa rahisi kukutana na fundi na akakutolea kitu aua kipimo cha saizi yako tofauti na jeans mpaka uende kiwandani na kwake sio rahisi kabisa.......PAMBAIKA


Wednesday 4 March 2015

[Alikiba:Huwa Sipendi Kuvaa Nguo Za Kubana Katika Show Zangu



Napenda sana kuvaa nguo zinazo uachia mwili wangu sababu huwa sipendi kubanwa pale ninapo kuwa busy hasa nikiwa natoa burudani pia hata viatu huwa navaa vilivyo na soli laini ili inifanye niwe flexible kwenye kudunda dunda nikiwa na cheza kwa upande wa gharama ya mavazi yangu ya show sijui ni kiasai gani huwa naangalia sana kipi kinanipendeza.Huwa napenda sana rangi nyeupe na nyeusi  




Sunday 1 March 2015

Miss CBE 2015 amepatikana Dar es salaam



Tunajua sifa ya kwanza uitwe Miss ni kuwa safi na kupendeza katika mavazi pia kichwa kiwe smart katika kujieleza na kujielewa sasa Neema sissamo alifanikiwa kupata taji hilo siku ya tarehe 28/02/2015 Jijini Dar-es-salaam. Check baadhi ya mitupio ya Pamba kwenye red carpet