bongo fleva super staa Nay Wa Mitego ‘Nyumbani Kwetu’ Video imetayarishwa na Director Joowzey.
Tuesday, 24 November 2015
Tuesday, 21 July 2015
CHRIS BROWN KUJA NA SNEAKER ZAKE MWENYEWE, KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA ASICS
Hit maker wa “Loyal” Chris brown kupitia mtandao wa Instagram ametangaza kuwa muda si mrefu ataachia viatu vyake mwenyewe “Sneaker” kwa ushirikiano na Kampuni ya ASICS ya Japan
Monday, 13 April 2015
Hayati Julius Kambarage Nyererere Aliingia kwenye vita ya maneno na Taifa la China kuhusiana na Suit Sisizo kuwa na kora(kaunda suit)
Nyerere alipoanza kuvaa
zile nguo zisizokuwa na kola yaani neckless shirts, hakukuwa na uhusiano wowote
na ziara yake ya China ya February mwaka 1965, na wala hakuiga kutoka kwa Mao
kama ambavyo wengi walidhania. Miaka hiyo kulikuwa na effort ya kutafuta vazi
ambalo ni identity ya waafrika, na wanasiasa ndio walikuwa msitali wa mbele
katika ubunifu. Vazi la kwanza kubuniwa na wanasiasa wetu lilikuwa ni blanket
la kujifunika kama ambalo linaonekana kwenye official portrait ya Nyerere ya
wakati huo kwenye picha ya hapa chini. Wanasiasa wengi barani Afrika
walijifunika mablanketi hayo, ambayo nadhani muasisi wake alikuwa Kwame
Nkurumah au Ahmed Sekou Toure. Zaidi ya Nyerere wanasiasa kadhaa wa Tanzania
pia walijifunga mablanketi hayo, kwa mfano Nyerere, Kambona Lusinde, n.k
Pamoja na kuvaa hayo mablanketi, miaka mitano ya
kwanza ya Nyerere madarakani alikuwa akichanganya mavazi ikiwamo business suit
pamoja na hayo mablanketi hayo kulingana na mazingira. Kwa mfano picha ya
cabinet yake ya kwanza ya mwaka 1962 na ile ya state visit yake Marekani mwaka
1963 alikuwa amevaa business suit kama zinavyoonekana hapa
Ingawa siku ya Muungano
bado alivaa business suit wakati wa kumkribisha Karume na wakati wa
kubadilishana hati za Muungano kama inavyoonekana hapa chini, ni katika kipindi
hicho hicho cha muungano ndipo alipoanza kuvaa hayo mashati ya neckelss kama
inavyoonekana kwenye picha ya cabinet yake ya kwanza ya mwaka 1964 hapa chini
kabisa
Official portrait ya
Rais Nyerere iliyotolewa wakati huo huo inamwonyesha wazi akiwa amevaa hicho
kineckless kama invyoonekana hapa chini. Hata Kawawa na Karume pia walikuwa
wamevaa hizo neckless shirts kwenye official portarits zao za mwaka 1964.
Kipindi hicho cha mwaka 1964 matumizi ya mablanketi kama nguo ya kiafrika yalianza kupungua sana na viongozi wengi wa Afrika ya Magharabi, ambayo ilitangulia kupata uhuru walikuwa wakivaa zaidi aina fulani ya kanzu ambazo ni kama jadi yao, na leo hii kanzu hizo zimekuwa maarufu sana kama nguo za kiafrika. Kanzu hizo hazikuwa na kola ( neckeless), kwa mfano nguo alizovaa Sekou Toure, Tafawa Balewa na Azikiwe kama ilivyo hapa chini hazina kola.
Kwa hiyo, ingawa hatujui ni
lini Nyerere na viongozi wenzake wa Tanzania walianza kuvaa hizo nguo za
neckless, ni wazi kuwa alianza kuzitumia kabla au mara tu baada ya Muungano,
April 1964 lakini ikiwa kabla hajasafiri kwenda China mwaka 1965. Kuna uhusiano
wa karibu sana katika uamuzi huo wa kuvaa mashati neckless na zile kanzu
neckless walizokuwa wakivaa "wanamapinduzi wa Afrika wakati huo",
ambao wengi wao walikuwa huko Afrika ya Magharibi.
Wakati Nyerere anatembelea
China mwezi Februari mwaka 1965, tayari alikuwa amevaa shati hilo neckless kama
anavyoonekana hapa wakati wa kusalimiana na Mao. Utamwona Nyerere alikuwa bado
ni kijana lakini amevaa hicho ki-neckless chake.
Na hata kwenye picha
aliyopiga na Charles De-gaule mwezi June mwaka huo huo 1965 hapa chini,
unamwona Nyerere amevaa kineckess chake. Baada ya Nyerere kutoka China, sinema
iliyohusu ziara yake huko China haikutoka mpaka mpaka mwishoni mwa mwaka 1965
akiwa tayari amesharudi kutoka ziara nyingine ikiwamo hii ya Ufaransa.
Aliendelea kutumia nguo hizi za neckless mpaka mwanzoni wa miaka ya sabini ambapo alianza kuvaa nguo zenye kola ambazo zilijulikana katika kipindi fulani kama Nyerere suit (kama kushindana na Kaunda suit za wakati huo.) Kuanzia hapo Nyerere akawa anachanganya hizo neckless suits, na hizo Nyerere suits zake. Mfano wake ni kama ionekanavyo hapa chini.
Aliendelea kuchanganya matumizi ya hizo Nyerere suits na Neckless suits hadi mwishoni wa maisha yake.
Mao alikuwa havai mashati yasiyokuwa na kola. Nguo za Mao pamoja na viongozi wote wa china zilikuwa zimeshonwa kuwa kama za kijeshi kama anavyoonekana hapo chini zikiwa na kola kubwa ya kutosha au ndogo ndogo lakini inayoweza kuwekwa nembo za kijeshi ikiwa lazima, kama anavyoonekana hapa chini.
Hata waziri wake mkuu, Chou En-Lai ambaye jina lake lilitumika kuziita hizo nguo neckless za Nyerere, pia alikuwa akivaa nguo zenye kola tu, kama anavyoonekana hapa chini.
Unaweza kuona tena katika ile picha ambayo Mao aliyopiga na Nyerere mwaka 1965 hapo na juu na ile aliyopiga naye tena mwaka 1972 pia hapa chini kuwa Mao alivaa shati lenye kola wakati Nyerere akiwa na shati lislokuwa na kola.
Ukiangalia tena kwa karibu zaidi, utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana baina ya Neckless za Nyerere na zile nguo za wachina kama inavyoonekana katika hii picha ya Sokoine akiwa na waziri mkuu wa China.
Nadhani wanasiasa wengi wakongwe Tanzania kama akina Mzee Malecela na Msuya ambao wamekuwa wakiendelea kuyavaa mashati yao neckeless freeely bila kuyaonea haya kwa vile nadhani wanajua wazi kuwa hawakuyakopi kwa Mao.
Nadhani maelezo hayo yanasaidia kuulewesha umma hasa wa wale waliozaliwa miaka ya karibuni kutambua kuwa lile vazi lislokuwa na kola la Nyerere halikuigwa na wala halikuwa na uhusiano wowote na China. Hatujui nani aliyelibuni lakini kwa vyovyote ni vazi lililobuniwa hapa hapa Tanzania kwani hakuna sehemu nyingine duniani lilikowahi kuvaliwa. Watu walioiga mavazi ya China kwa hapa Afrika labda ni pamoja na kwame Nkurumah, na Mengistu Haire Mariam kama wanavyoonekana hapa chini.
Wednesday, 8 April 2015
Kesi Ya Kanye West,Kumshambulia Papalazzi Yafutwa
Kesi ya mwana mitindo
Kanye west yafutwa,Ilikuwa katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.West alishtakiwa kwa kosa la kumshambilia paparazzi Daniel Ramos Mwaka 2013 ila kwa sasa
wameyamaliza kwa kushikana mikono
alietoa taarifa hiyo ni wakili wa paparazzi Daniel Ramos anaye fahamika kwa
jina la Gloria Allred aliandika maelezo hayo jana jumnne kuwa kesi hiyo
imemalizika na kwamba Designer huyo alimuomba msamaaha mteja wangu.Wakili Gloria
Allred alitumia picha ya Kanye West akitabasamu wakati akishikana mkono na paparazzi
Daniel Ramos
Sunday, 22 March 2015
Uliwahi kuvutiwa na uvaaji wa Pharrell Williams? Basi ile style yake imempa TUZO !!
Nyingine ambayo huenda hujaipata ni ishu ya Pharell Williams kutajwa kuwa ndiye mwanamuziki aliyeshinda CFDA Fashion Icon Awards ambapo ushindi huo unatokana na jinsi style yake imekuwa maarufu na kushawishi watu wengi duniani......Pharell atapewa Tuzo hiyo June 1 2015, lakini toka jina lake limetajwa kama mshindi mitandao imeendelea kuandika na kuuchambua huu ushindi wa Pharell
Wapo walioandika eti kawa mshindi kwa sababu ya ile kofia ambayo anapendelea kuvaa!
Mastaa wengine waliowahi kushinda Tuzo hii ni pamoja na Rihanna na Lady Gaga.
Sunday, 15 March 2015
Hanscana Ame Copy NaKu Pest Idea Ya Wimbo Wa Jux Toka Xo(Nisher)
Director Nisher aliye fanya ngoma kadhaa za video ikiwemo Xo ya Joh Makini hivi karibuni alitoa malalamiko juu ya video mpya ya Jux iliofanywa na Director Hanscana kuwa hajatumia mawazo yake na ufundi zaidi ya kuamisha mawazo toka kwenye video ya Xo ilikuwa imefanyika chini ya mikono ya nisher
Aliamua kuthibitisha hayo kwa kupost baadhi ya picha kwenye mtandao wa picha(Instagram) na kuonesha alicho kuwa anakilalamikia
Friday, 13 March 2015
Labda hii ni mpya kwako.. mbwa anayetembea na kuvaa kama binadamu yani.. Kuna video
Mbwa kwenye pozi zake na mavazi kama tu binadamu, pata picha unakutana naye barabarani halafu anatembea tu kama binadamu kwa miguu miwili.
Wachina hawajashindwa kitu, hii imezua mjadala katika mitandao.. waliobahatika kukutana naye barabarani walijikuta wakigeua vichwa kumcheki, imetokea China.
Mbwa huyo amevalishwa kofia, shati na sketi, mgongoni amebeba begi kama mwanafunzi wa shule, halafu anakatisha zake mtaani poa kabisa yani.
Mtu anaemfuga mbwa huyo anaitwa Zhu, amesema ametumia muda wa mwezi mmoja kumfundisha mbwa huyo kutembea kwa miguu miwili kama binadamu, ana uwezo wa kutembea kilomita mbili wima kama mwanadamu.
Zhu anasema alianza kufundisha mbwa kama njia ya kujifurahisha miaka 20 iliyopita, baada ya kuona mafanikio aliona aendelee kufanya hivyo kwa kuwafundisha mbwa wengine wengi.
Subscribe to:
Posts (Atom)